Urambazaji

Masharti ya matumizi

Urambazaji

Masharti haya yanahusiana na nini?

Masharti haya ya matumizi yanaelezea matumizi yanayoruhusiwa kwa ajili ya huduma ya ZanzibarLII inayopatikana kwa https://new.zanzibarlii.org/ na maeneo yake madogo.

Sisi ni nani, na jinsi ya kuwasiliana nasi?

ZanzibarLII is developed under the auspices of the Judiciary of Zanzibar and publishes the law of Zanzibar for free online access to all. ZanzibarLII promotes the rule of law and access to justice in Zanzibar. Unaweza kuwasiliana nasi kwa barua pepe kwa info@zanzibarlii.org au kwa kujaza fomu hii.

Kwa kutumia huduma ya ZanzibarLII unakubaliana na masharti haya

Kwa kutumia huduma ya ZanzibarLII, unathibitisha kuwa unakubali sheria na masharti haya na unakubali kuyafuata.

Matumizi mazuri na ya kuridhisha

Ni lazima utumie huduma kwa kuwajibika kwa kutofanya maombi mengi. Ili kudumisha uadilifu wa huduma kwa kila mtu, tunaweza kuzuia au kuzima matumizi ya huduma kutoka katika baadhi ya anwani za IP, kwa kufanya maombi mengi sana.

Sisi ni shirika linalofadhiliwa na uhamishaji mkubwa na wa mara kwa mara unaathiri gharama zetu na kuhatarisha uendelevu wa huduma. Kuna njia bora zaidi za kuweza kupata data zetu kwa wingi. Tafadhali tutumie baruapepe kama ungependa kukupata data zetu kwa wingi.

Kutafuta na kupanga

Unaweza kupata huduma ya ZanzibarLII kupitia tovuti, au kupata data kupitia API zetu.

Tunazuia upangaji kutoka nje wa nyaraka kwa roboti za injini tafuti au buibui. Lazima ufuate maelekezo katika mafaili ya roboti.txt katika: https://new.zanzibarlii.org/robots.txt

Tunaweza kuzuia au kuzima matumizi ya huduma kutoka kwa anwani fulani za IP, ikiwa zinaonekana kuwa zinaunda faharasa ya injini tafutizi.

Eneo

ZanzibarLII hukusanya kesi za mahakama, sheria, hati za Umoja wa Afrika, majarida, vitabu na nyenzo zingine kupitia ushirikiano na mashirika ya kikanda, kiserikali, kitaaluma na yasiyo ya kibiashara na wakati mwingine watu binafsi.

Tunajitahidi kuhakikisha viwango vya ubora wa juu kwenye nyaraka zote zilizochapishwa kwenye jukwaa. Ambapo uthibitishaji haukuwezekana, hii itaonyeshwa kwenye hati inayohusika.

Makosa na uondoaji

Tunaskani na kuweka kidijiti nyaraka zilizo nyingi zinazopatikana kwenye tovuti za ZanzibarLII na washirika wa LII. Tunatumia programu Inayobadili Picha iweze kusomeka (OCR) ili kubadilisha nyaraka hizi kuwa maandishi yanayosomeka na kunaweza kuwa na makosa yanayoletwa na mchakato huu.

Tafadhali wasiliana nasi iwapo utapata hitilafu katika nyaraka zozote zilizochapishwa na tutazirekebisha ndani ya muda muafaka.

Zuio

Ingawa tunafanya kila jitihada kuthibitisha taarifa na kujumuisha chanzo na historia ya nyaraka zilizochapishwa kwenye huduma hii, unapaswa kutambua kuwa taarifa kwenye ZanzibarLII ni:

  • si lazima kuwa ya kina, kamili, sahihi au ya kisasa;
  • wakati mwingine inahusishwa na tovuti za nje ambazo ZanzibarLII haina udhibiti na ambapo ZanzibarLII haiwajibiki;
  • si ushauri wa kitaalamu au wa kisheria (ikiwa unahitaji ushauri maalumu, unapaswa wakati wote kushauriana na mtaalamu mwenye sifa anayefaa).

ZanzibarLII na Laws.Africa, wafanyakazi wake, na wakandarasi wake hawatawajibika kwa madhara yoyote ya kifedha au mengine yanayotokana na matumizi ya taarifa au data iliyomo kwenye tovuti hii, ikiwa ni pamoja na matumizi yasiyofaa, yasiyo sahihi au ya udanganyifu wa taarifa au data hizo.

ZanzibarLII hairuhusu utegemezi, wala kukubali kuwajibika kwa taarifa inayoitoa. ZanzibarLII inafanya kila jitihada kutoa huduma ya ubora wa hali ya juu. Hata hivyo, si ZanzibarLII wala watoa data kwenye ZanzibarLII, wanaotoa uhakika, ahadi au dhamana yoyote kuhusu usahihi, ukamilifu au hali ya upya wa taarifa iliyotolewa. Watumiaji wanapaswa kuthibitisha taarifa kutoka katika chanzo kingine ikiwa ni ya umuhimu wa kutosha kwao kufanya hivyo.

Viungo vya Hypertext kwenye ZanzibarLII (mara nyingi) huingizwa na ZanzibarLII, sio watoa data. Uingizaji kiotomati wa viungo vya hypertext kwenye ZanzibarLII inamaanisha kuwa viungo havitakuwa vya kina au sahihi kwa namna zote. Si ZanzibarLII wala watoa data wake, wanatoa uhakika, ahadi au udhamini wowote kuhusu viungo vya hypertext.

Hakimiliki na Utoaji leseni

Unaweza kutumia na kutumia tena maudhui ya sheria ya msingi na ufafanuzi wake kwenye ZanzibarLII chini ya masharti ya leseni ya Creative Commons Attribution-NonCommercial 4.0 International. Chini ya leseni hii, unaweza kutumia, kutumia upya na kusambaza upya kazi kutoka ZanzibarLII bila malipo, ili mradi umetoa kwa ZanzibarLII kama chanzo chako na matumizi yako si kwa manufaa ya kibiashara.

Makusanyo maalumu kwenye ZanzibarLII yanaweza kupewa leseni chini ya leseni zinazoruhusiwa zaidi. Mifano ya makusanyo hayo ni hati za Umoja wa Afrika ambazo hazijahaririwa, sheria za kitaifa na kikanda na magazeti ya serikali. Angalia ukurasa wa kwanza wa kila mkusanyiko kwa maelezo maalumu ya utoaji leseni.

Matumizi ya maandiko ya kisheria yaliyochapishwa na ZanzibarLII yanaweza kuwa chini ya masharti ya ziada yaliyowekwa na mahakama, vyombo vya kanda na vya serikali, na wachapishaji wanaodai haki za milki ya ubunifu zinazohusiana na nyaraka. ZanzibarLII inafanya jitihada za kuonyesha kuwepo kwa masharti ya ziada kwenye kurasa za hifadhidata husika. Bado, Watumiaji wanabaki na jukumu la kuangalia kama matumizi yao ya nyaraka yameidhinishwa.

ZanzibarLII inahifadhi haki za milki ya ubunifu kwenye jina, michoro ya tovuti na usanifu wa tovuti ya ZanzibarLII.

Faragha

Taarifa kuhusu matumizi ya ZanzibarLII

ZanzibarLII inakusanya taarifa ambazo zinabainisha, kwa kila ukurasa unaofunguliwa kwenye ZanzibarLII, utambulisho wa mtandao wa mashine ambayo imefunguliwa. Tunatumia Google Changanuzi na programu ya ndani kutekeleza utendaji huo.

ZanzibarLII inahifadhi taarifa hizi za matumizi kwa madhumuni ya uchanganuzi wa mtandao, uchanganuzi wa matumizi na utafiti katika mifumo ya utumiaji ili kuboresha huduma za ZanzibarLII. Upatikanaji na utumiaji wa taarifa hizi unapatikana kwa Google Changanuzi tu, menejimenti na wafanyakazi wa ZanzibarLII, na kwa watafiti wanaofanya kazi kwenye miradi ya ZanzibarLII na kulingana na makubaliano ya kufuata Masharti haya.

ZanzibarLII ina haki ya kukusanya taarifa nyingi zaidi kuliko ilivyoelezwa hapo juu (i) kuhusu jaribio lolote la kufikia ZanzibarLII ambalo linazua masuala ya usalama (na, pale inapobidi, kufichua kwa mamlaka husika); na (ii) kwa uchanganuzi wa mtandao mara kwa mara.

Taarifa binafsi zilizomo katika hifadhidata ya ZanzibarLII

Taarifa binafsi katika kesi za mahakama

ZanzibarLII inachapisha makusanyo ya kina ya maamuzi ya mahakama kwa idhini ya vyombo vya umma vinavyohusika. Usambazaji wa hukumu za kielektroni unaendana na kanuni ya mahakama ya wazi, iliyoanzishwa ili kuhakikisha kutopendelea na uwazi wa mchakato wa mahakama kwa kuruhusu upatikanaji wa rekodi za mashtaka ya mahakama, ikiwa ni pamoja na hukumu. Kwa hiyo, ZanzibarLII inafanya kazi kwa kufuata kanuni ya msingi kwamba wananchi wote na mashirika wanapaswa kupewa bure, bila masharti na kupata bila vikwazo maandiko ya msingi ya kisheria.

ZanzibarLII inajitolea kufuatilia na kufuta kutoka katika taarifa binafsi za hukumu zilizochapishwa kama inavyoelekezwa na sheria au amri maalumu ya mahakama. ZanzibarLII inabaki na haki ya kuondoa maelezo ya binafsi kutoka katika hukumu kwa hiari yake inapowezekana bila kupotosha maana na muktadha wa waraka.

Taarifa binafsi kwenye magazeti ya serikali

Majarida ya serikali na majarida rasmi ni machapisho rasmi ya majimbo yanayochapisha. Sheria inaamuru kwamba taarifa fulani za kibinafsi zinapaswa kutangazwa kwa umma kupitia gazeti la serikali na idara za serikali zinaweka matangazo haya ya umma kwenye gazeti la serikali kwa nia ya yaliyomo kupatikana kwa umma.

ZanzibarLII haiwezi kujiondoa kutoka katika usambazaji, kuhaririwa au kurekebisha gazeti la serikali.

Ufuatiliaji wa kiotomati

ZanzibarLII hufanya ufuatiliaji wa kiotomati na, inapohitajika, kuondoa utambulisho wa hukumu kabla ya kuchapishwa na haihakikishi kuwa maandiko yote nyeti yameondolewa kwa njia sahihi.

Iwapo una wasiwasi juu ya taarifa binafsi zilizochapishwa kwenye tovuti ya ZanzibarLII, tafadhali wasiliana nasi.

Matumizi yako salama ya taarifa binafsi

ZanzibarLII watumiaji wanapaswa kutambua kwamba kuna vikwazo vya kisheria juu ya matumizi, uchapishaji na usambazaji wa baadhi ya taarifa za kibinafsi katika hifadhidata ZanzibarLII . Ni wajibu wa watumiaji ZanzibarLII kuzingatia sheria za nchi.

Haki ya kurekebisha Masharti haya ya Matumizi, Hakimiliki na Faragha

Tuna haki ya kurekebisha masharti haya ya matumizi, hakimiliki, na taarifa za faragha na usalama wakati wowote. Marekebisho yote yatawekwa kwenye tovuti hii. Isipokuwa imeelezwa vinginevyo, toleo la sasa litachukua nafasi na kubadilisha matoleo yote ya awali ya hati hii.

Ikiwa una maoni au mapendekezo yoyote kuhusu sera hii, tafadhali wasiliana nasi.

Tarehe ya taarifa: 14 Novemba 2022